Kwaheri bwana Gakuru, Pema Mola akulaze

Wahome Gakuru

Wahome Gakuru

KWAHERI GAVANA GAKURU!!

Ninalianza shairi, kwa majonzi ya dhahiri,
Kwa kuwa tena si siri, ajali zimekithiri,
Zaua kwa utitiri, hii sasa ni hatari,
Kwaheri bwana Gakuru, Pema Mola akulaze

Musa ah! naliandika, Kalamu wino machozi
Najikaza kuishika, Nalibuni kwa majonzi
Maini yanikatika, Katutoka kiongozi
Kwaheri bwana Gakuru, Pema Mola akulaze

Majonzi yametukumba, Kenya Yetu Kwa dhiki
Ametutoka ja vumba, Kifo hakitabiriki
Karudi kwake Muumba, Alotaka afariki
Kwaheri bwana Gakuru, Pema Mola akulaze

Twakukumbukia wema, Ulotenda me kithiri
Na mengi uliyosema, Hatuwachi kukariri
Mola akulaze pema, Peponi akusitiri
Kwaheri bwana Gakuru, Pema Mola akulaze

Na Musa Methali!

Mutahi Kahiga To Be Sworn In Following The Demise Of Nyeri Governor

Hits: 1538
Share